• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mkinga District Council
Mkinga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Livestock and Fishary
      • Works and Fire Recure
      • Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari Mawasiliano na Uhusiano
      • Ugavi
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Legal
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma wa Maji
    • Huduma ya Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Maktaba ya Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Matukio
    • Habari
    • Matukio

MAKARANI WAOMNGOZAJI WAPIGA KURA WAASWA KUWA WAADILIFU

Posted on: October 25th, 2025

Na: Nassoro Rashid – Mkinga, Tanga

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mkinga, Ndugu Juma Jackson Hamadi, amefungua rasmi mafunzo ya siku moja kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura, akisisitiza umuhimu wa uadilifu, uzingatiaji wa sheria, na uwajibikaji wa hali ya juu katika utekelezaji wa majukumu yao kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Akizungumza katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Hamadi alisema mafunzo hayo ni sehemu muhimu ya maandalizi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru, wa haki, wenye uwazi na amani.

“Dhamana mliyopewa ni kubwa na nyeti. Mnapaswa kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni na maelekezo ya Tume. Huu si wakati wa majaribio, bali ni wakati wa kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu,” alisema Hamadi.

Alifafanua kuwa jumla ya makarani waongozaji 339 wanashiriki mafunzo hayo, ambapo watasambazwa katika vituo 295 vilivyopo katika kata 22 za Wilaya ya Mkinga. Watendaji hao, alisema, ndio watakaokuwa kiungo muhimu kati ya Tume na wananchi siku ya kupiga kura.

“Ninyi ndio mnakutana ana kwa ana na wapiga kura, hivyo hakikisheni mnatenda kwa unadhifu, lugha nzuri, na kutoa huduma bora kwa kila mpiga kura bila upendeleo. Wapeni kipaumbele wapiga kura wenye mahitaji maalum,”. Alisema Ndugu Hamadi.

“Tangu siku ya uteuzi wenu, ninyi ni watumishi wa Tume. Simamieni viapo vyenu, mtunze siri za uchaguzi na fanyeni kazi kwa maslahi ya Taifa letu,” alisisitiza

Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Mafunzo, Ndugu Rajabu Mangala, alisema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwani yanawapa makarani uelewa wa kina kuhusu utaratibu wa upigaji kura, uhesabuji wa kura na utunzaji wa nyaraka za uchaguzi. Alisisitiza kuwa uelewa huo utasaidia kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu, uwazi na ufanisi mkubwa.

Naye, Bi. Mwanaidi Jumaa Mashango, akizungumza kwa niaba ya makarani wenzake, alisema wamepokea vyema mafunzo na maelekezo waliyopewa, na wako tayari kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uaminifu mkubwa.

“Tumejifunza kwa kina majukumu yetu na tunakwenda kufanya kazi kwa uadilifu, tukizingatia sheria na maelekezo yote tuliyopewa. Tutaenda kutumikia Taifa kwa uaminifu na bidii,” alisema Bi. Mwanaidi.

Hamadi aliongeza kuwa kwa kipindi chote cha uchaguzi, watendaji hao wanawajibika moja kwa moja kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na si mamlaka nyingine yoyote.

Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA October 16, 2023
  • HATI MILIKI ZA ARDHI ZILIZOKAMILIKA WILAYA MKINGA December 04, 2022
  • KUSAFISHA MAENEO KWA WAMILIKI WA VIWANJA MKINGA August 12, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA July 18, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA KWA AMANI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

    October 23, 2025
  • MAKARANI WAOMNGOZAJI WAPIGA KURA WAASWA KUWA WAADILIFU

    October 25, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

Angalia zaidi

Kurasa za Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Habari

Kurasa Mashuhuri

  • OR- TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Salary slip portal
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Taifa
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Kasera, Tanga -HorohoroRoad

    Postal Address: P O Box 6005 Tanga

    Simu: +255 027-2660501

    Simu: +255 684 625 299

    Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Huduma

Mkinga dc @ 2017