• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mkinga District Council
Mkinga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Livestock and Fishary
      • Works and Fire Recure
      • Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari Mawasiliano na Uhusiano
      • Ugavi
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Legal
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma wa Maji
    • Huduma ya Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Maktaba ya Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Matukio
    • Habari
    • Matukio

"BILA UMOJA NA MSHIKAMANO HATUTAWEZA KUITENDEA HAKI IMANI NA TULIYOPEWA NA WANANCHI"-MHE. GILBERT KALIMA

Posted on: December 3rd, 2025

"BILA UMOJA NA MSHIKAMANO HATUTAWEZA KUITENDEA HAKI IMANI TULIYOPEWA NA WANANCHI" - MHE. GILBERT KALIMA

Na: Nassoro Rashid - Mkinga

Desemba 3, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Gilbert Kalima, ametoa wito mzito kwa Baraza Jipya la Madiwani kuhakikisha umoja, ushirikiano na mshikamano vinakuwa nguzo kuu ya utekelezaji wa majukumu yao katika kipindi kipya cha uongozi.

Akihutubia katika Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani, Mhe. Kalima amesema kuwa bila kuungana na kufanya kazi kwa pamoja, viongozi hawataweza kuitendea haki imani kubwa waliyopewa na wananchi.

Ameonya kuwa endapo kutakuwepo mgawanyiko ndani ya Baraza, mambo muhimu ya maendeleo hayatapitishwa na hatimaye matarajio ya wananchi yatadumaa.

“Bila umoja na mshikamano, tutakuwa na mabaraza mawili au matatu ndani ya kikao kimoja. Tutapinga wenyewe kwa wenyewe na hatutafikia malengo wanayotamani wananchi wetu,” amesema.

Aidha, Mhe. Kalima amesisitiza umuhimu wa madiwani kuendeleza mafanikio makubwa ya halmashauri katika kuongeza mapato ya ndani. Amekumbusha kuwa mwaka 2020 Halmashauri ya Mkinga ilikuwa inakusanya milioni 800 pekee, lakini kwa nguvu ya pamoja, mapato hayo yamefikia takribani shilingi bilioni 3 katika mwaka uliopita wa fedha.

Amesema kuendelea kupanda kwa mapato kutategemea kiwango cha ushirikiano baina ya madiwani, watendaji na viongozi wa kisiasa.

“Tukikosa mshikamano tutarudi nyuma. Kwani bila ya umoja na mshikamano hatutaweza kuitendea haki imani tuliyopewa na wananchi, Hii tusiruhusu kamwe,” amesisitiza

Sanjari  Mkuu huyo wa wilaya ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji, Watendaji na Idara zote kwa kuendelea kuihudumia Mkinga kwa umahiri katika kipindi chote ambacho Baraza la Madiwani lilikuwa limevunjwa.

Amesema taarifa walizowasilisha mbele ya baraza ni ushahidi wa kazi kubwa na ya mfano inayofanywa na watumishi wa Halmashauri.

Akigusia fedha zinazotolewa na serikali kuu, ikiwemo milioni 800 kwa uendelezaji wa Hospitali ya Wilaya, Mhe. Kalima amesisitiza kuwa jukumu la madiwani sasa ni kufuatilia na kusimamia matumizi ya fedha hizo kwa mujibu wa malengo yaliyokusudiwa.

“Fedha hizi zikitumika sawa, tutakuwa tumewatendea haki wananchi. Tusipokuwa wamoja tutaathiri usimamizi wake,” amesema.

Pia Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa amani na utulivu ndivyo vinavyofanya shughuli zote za maendeleo ziendelee. Ameitaka jamii na viongozi wote kuwa walinzi wa amani, akisema bila utulivu hakuna uwezekano wa kuboresha huduma za jamii kama maji, afya, elimu na barabara.

“Amani ndio msingi wa maendeleo yote. Tuihifadhi, tuilinde na tuihubiri kwa nguvu zote,” amesema.

Mhe. Kalima ametamatisha kwa kuwataka viongozi wote wa Mkinga kutanguliza maslahi ya wananchi na kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na moyo wa kujitoa kwani umoja wa viongozi ndio shukrani ya kweli wanayoweza kuirudisha kwa wananchi waliowachagua.

Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA October 16, 2023
  • HATI MILIKI ZA ARDHI ZILIZOKAMILIKA WILAYA MKINGA December 04, 2022
  • KUSAFISHA MAENEO KWA WAMILIKI WA VIWANJA MKINGA August 12, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA July 18, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA KWA AMANI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

    October 23, 2025
  • MAKARANI WAOMNGOZAJI WAPIGA KURA WAASWA KUWA WAADILIFU

    October 25, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

Angalia zaidi

Kurasa za Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Habari

Kurasa Mashuhuri

  • OR- TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Salary slip portal
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Taifa
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Kasera, Tanga -HorohoroRoad

    Postal Address: P O Box 6005 Tanga

    Simu: +255 027-2660501

    Simu: +255 684 625 299

    Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Huduma

Mkinga dc @ 2017